Uchambuzi: Tuhuma dhidi ya Nyama Nyekundu, Wakati gani inakuwa Salama na Mbaya kiafya

Najua hata wewe umekuwa ukikutana na utata mkubwa sana kuhusu nyama aina mbalimbali, na kuna mtizamo hasi kwa jamii kuhusu nyama kama nyama ya ng’ombe,kondoo,mbuzi nk wakizipa jina nyama nyekundu.

Upande wa pili nyama kama kuku,samaki ndege zimekuwa na mtizamo mzuri katika jamii kwamba ni nyama nzuri zaidi ya nyama nyekundu.

Huu hapa ndio ukweli kuhusu aina mbalimbali za nyama, nina muda wa miaka zaidi ya 5 nikifuatilia kuhusu sayansi ya nyama na nimekuwa nikikutana na mshangao mkubwa sana pale unapomwambia mtu kuhusu ukweli wa nyama.

Na inakuwa ni vigumu kumsaidia  kuhusu fikra potofu alizo jengewa,Ndani ya kitabu cha sayansi ya mapishi tulijifunza mengi sana kuhusu nyama na huu ni mwendelezo, tafadhari nakushauri usome kitabu hicho cha awali kabla hujasoma hapa ili unielewe vizuri kuhusu mwendelezo wa mada hii.

 

No automatic alt text available.

 

Kusoma makala mbalimbali za Uchambuzi kama hizi Pakua Lishe Bora App Bonyeza: LISHE BORA HEA APP  

Swali la kwanza: Je wekundu wa nyama Dr Boaz ndio unafanya nyama ya ng’ombe,mbuzi, kondoo iwe mbaya kiafya kwa matumizi ya chakula cha binadamu?

Jibu: Hapana, wekundu wa nyama hizi hauashirii ubaya wa nyama husika. Kuna watu hufikiria hivyo kwamba labda ule wekundu ndio ubaya wa nyama. Nyama kuwa nyekundu ni sifa mojawapo ya wanyama hawa kama ng’ombe,mbuzi, kondoo kuweza kuishi katika mazingira yao na kujipatia chakula. Wekundu wa nyama ni kwa sababu ya kiwango kingi cha myoglobin ambayo inapatikana katika misuli ya mnyama na hii husaidia kunasa oksijeni na kutoa oksijeni pale inapohitajika kutengeneza nishati katika misuli kumwezesha mnyama husika kutembea,kukimbia,kusimama na matendo yote kama kiumbe hai.

Mfano ng’ombe, mbuzi, kondoo muda wote misuli yao inafanya kazi ngumu hata kupumzika hupumzika kwa kufanyika , ndio maana misuli ya wanyama hawa ina kiwango kingi cha myoglobin la sivyo wasingeweza kustahimili mazoezi wanayo fanya, muda wote misuli ya wanyama hawa ipo kazini ndio maana ina kiwango kingi cha myoglobin kuwezesha hilo.

Samaki huwa ana kiwango kidogo sana cha myoglobin kwa sababu yeye muda wote huwa anaogoelea kwenye maji na kwa maana hio hakuna uhitaji mkubwa wa oksijeni ndio maana hata kiwango cha myoglobin kipo kidogo sana. Hata kuku muda mwingi kuku anakuwa anatembea kwa hio mapaja na miguu inakuwa kidogo na kiwango kikubwa cha myoglobin (Chembe nyekundu) na ndio hufanya miguu na mapaja iwe ni nyama nyekundu wakati mabawa ya kuku na kifua ni nyama nyeupe kwa sababu misuli yake haitumiki mara kwa mara.

Kwa lugha nyepesi wekundu wa nyama husika ni sifa ya kiumbe kuweza kustahimili zoezi lake la kila siku na kumwezesha kuishi katika mazingira yake, lakini sio kweli kwamba myoglobin ni sumu katika mwili wa binadamu pale ulapo hadi sasa hakuna sehemu yoyote ambapo imehusishwa kusababisha hilo.

 

Swali la pili: Je kati ya nyama ya kuku na ng’ombe ipi ni nyama yenye ubora unapozungumzia viini lishe ndani yake na afya ya mwili kwa nyakati hizi?

Kwa haraka haraka jibu la mtu yeyote litakuwa ni nyama ya ng’ombe ndio sio nzuri kwa binadamu, lakini ukweli ni kwamba nyama ya ng’ombe iko juu katika vigezo vyote kiafya ukilinganisha na nyama ya kuku.

Unachotakiwa kufanya ni kuchagua nyama ya ng’ombe anayechunga nyasi sio anayelishwa mashudu ya mahindi au nafaka mbalimbali kama ng’ombe wanaofugwa katika teknolojia ya kisasa sana siku hizi kwani utofauti mkubwa wa ng’ombe anayechunga nyasi huwa ina kiwango kingi cha omega 3 ambacho tunashauriwa kuongeza matumizi yake, pia huwa ina kiwango kidogo cha omega 6 ambacho huwa tunashauriwa kupunguza kiafya, Lakini nyama ya ng’ombe asiyechunga nyasi anayelishwa nafaka tupu ana kiwango kidogo sana cha omega 3 ambayo tunashauriwa kuongeza na huwa na kiwango kingi cha omega 6 ambayo hushauriwa  kupunguza. Unapokuja kwenye kuku na nyama ya ng’ombe anayechunga nyasi, nyama ya ng’ombe itabaki kuwa juu kiafya na kwa mtizamo wa kulinda mishipa ya damu na moyo kwa sababu ina kiwango kingi cha omega 3 na kiwango kidogo cha omega 6 wakati kuku ina kiwango kidogo cha omega 3 na kiwango kingi cha omega 6.

Chapisho ambalo lilitolewa na Taasisi ya Wataluma wa lishe Australia,Chuo kikuu hollogong,Chapisho hilo lilitolewa na Profesa PG William amehusisha moja ya jedwali likionesha uwiano wa omega 3 na omega 6 ( Ratio ya omega 3/omega 6) kwenye gram 100 ya nyama aina mbalimbali nyekundu na nyeupe, Nyama ya ng’ombe uwiano wake ulikuwa 0.45, wakati kuku ikiwa ni 0.13, Samaki 3.6 na mafuta ya samaki yaliongoza kwa kupata uwiano wa 10.42. Kwa lugha nyepesi ukitaka kuchagua nyama aina gani ina kiwango kingi cha mafuta mazuri tunayo shauriwa kutumia na hulinda na kutibu majeraha ya  mishipa ya damu itakuwa kwanza, Mafuta ya samaki,inafuata nyama ya samaki,inafuata nyama ya ng’ombe na nyama ya kuku ipo chini sana.

Moja ya chapisho lingine ambalo linaonesha jinsi gani ubora wa nyama huharibiwa na mfumo jinsi gani wanyama tunao wafuga tunavyo wapatia chakula chao,Chapisho hilo (PIP Ponte, JAM Prate Restricting the Intake of a Cereal-Based Feed in Free-Range-Pastured Poultry:, 2008) linaonesha kwamba wanyama wengi wa kufuga kwa kuwanenepesha kwa nafaka na sio nyasi nyama yake sio bora kama wale wanaochunga nyasi. Nyama ya kuku imeonesha kuwa na kiwango kingi cha omega 6 na kiwango kidogo cha omega 3 kutokana na  uhusiano ulio oneshwa kwa kutumia jedwali. Sababu iliyotolewa ni kwa sababu chakula kikuu cha kuku ni nafaka, na mashudu ya nafaka. Ndio maana kuku wanao achwa na kujichunga wenyewe kwa kula panzi,majani na nafaka kidogo huwa nyama yake inatofautiana na kuku wengine wanaofugwa kwa vyakula maalumu vyenye mashudu ya nafaka tupu kwa Kuzingatia  kiwango cha omega 3.

Pia siku zote tumekuwa tukiogopa nyama nyekundu kwa sababu ya nadharia ya kwamba nyama nyekundu sio nzuri huleta magonjwa ya moyo, kansa nk Lakini ukweli ni kwamba aliyetufanya tujenge woga huu ni bwana Ancel Benjamin keys alitengeneza Nadharia yake ya kwamba “Mafuta yanayo ganda hubadilishwa mwilini na kuwa cholesterol” na akachapisha. Tangu miaka ya 1950s tafiti hii itoke imezuia mjadala mpana sana kwa wanasayansi wakihoji, mbona hakuna sehemu yoyote kisayansi inayo onesha mabadiliko ya mafuta yanayo ganda kuwa cholesterol? Kosa ambalo Keys alifanya katika kufikiria kwake ni “Hakukuwa na sayansi yoyote yaani yeye alitengeneza nadharia na kutaka kuihakiki, ingawaje mwanzoni alionekana ndiye mkombozi amegundua chanzo halisi cha magonjwa ya moyo, lakini kwa sababu mlipuko wa magonjwa ya moyo bado unakuwa kwa kasi mbali na kuepuka kwetu vyakula hivyo na mbali na kuishusha cholesterol kwa kutumia dawa kali zenye hata athari nyingi kuliko faida”. Majopo ya wanasayansi wamekuwa wakilaumu sana Nadharia ya Keys kwamba “Ndio iliyochangia jamii kuugua kiasi hiki magonjwa yatokanayo na ulaji wa kupindukia wa sukari wakati binadamu anakimbia vyakula vya mafuta” Ingawaje kuna wanasayansi wanaibuka kwa kusema Ancel Keys hatakiwi kulaumiwa, yeye alifanya tu tafiti hakusema “Tutengeneze maziwa ambayo hayana mafuta,hakusema tule nyama ambazo hazina mafuta,hakusema tutoe kiini chake hakusema tule vyakula hivi vyenye shehena kubwa ya sukari kwani hata kwenye tafiti yake sukari ilionesha kuleta athari kubwa sana na alitoa ripoti hio, Wengine husema viwanda vya vyakula na utandawazi wa viwanda ndio wakulaumiwa lakini sio mwanasayansi Ancel keys” soma chapisho lake (KD1, Pett; J2, Kahn; Ancel Keys and the Seven Countries Study, White Paper An Evidence-based Response to Revisionist Histories, 2017).

Mbali na hivyo tafiti mbalimbali zimekuwa zikifikia hitimisho kwamba lehemu sio chanzo cha magonjwa ya moyo, ndio maana zaidi ya nusu ya watu wanaopata shambulio la moyo huwa wana kiwango cha cholesterol au lehemu kiwango cha kawaida kabisa ndani ya kipimo unacho shauriwa kiafya.

Hadi sasa kuna tafiti nyingi zinazidi kumiminika kuonesha kwamba kuna vihatarishi ambavyo huleta majeraha katika mishipa ya damu,mwili na kusababisha kuvimba kwa mishipa ya damu na mwili, na matukio kama hayo husababisha cholesterol kwenda kurundikwa kwenye kuta za mishipa ya damu.

Kwa lugha nyingine “Bila majeraha kutokea yaani endothelial inflammation, cholesterol haiwezi kuleta ubaya wowote” ndio maana mwili wa binadamu umetengenezewa uwezo wa kuzalisha cholesterol zaidi ya asilimia 85 na ndio maana nyama imekuwa chakula kikuu hata kabla ya Mapinduzi ya viwanda kipindi hicho bibi zetu wanalipa shamba la nafaka dogo sana,maharage kidogo sana tunachakata kwa kusaga na mawe, leo hii utaweza kusaga mahindi au mtama kwa mawe kuwatosha watu 10 katika familia? Huwezi na ni ishara ya kwamba hakikuwa chakula kikuu cha nishati na nguvu kwa binadamu, Ndio maana nyakati hizi nyama inavyotengenezewa picha mbaya ukweli wa nyuma unagoma kuyahakiki hayo yote.Uwiano wa omega 3 na omega 6 sasa unazidi kushamiri kuwa ni kiashiria kikubwa sana cha binadamu kupata shambulio la moyo, hata shirika la afya duniani linashauri sana tuongeze matumizi ya omega 3 yaani DHA,EPA na ALA na tupunguze matumizi ya omega 6 kwa maana hio ukitupilia mbali nadharia ya cholesterol huleta magonjwa ya moyo, nyama ya kuku haiwezi kuwa bora zaidi ya nyama ya ng’ombe maana ukitizama uwiano wa omega 3 na omega 6 kwenye kuku ni mdogo sana.

Dhana ya kwamba nyama ya kuku ni nzuri kuliko ya ng’ombe ukisoma kwa kina hutakuja kukubaliana na hilo hata kidogo.

Sijakwambia basi ule nyama pekee hata kilo 2 kwa siku moja hapana, lakini unapo ambatanisha nyama ya ng’ombe anayechunga nyasi na mboga za majani zenye rangi tofauti tofauti, matunda aina mbalimbali ,nyama inaweza kukusaidia kiafya na haina madhara kwa mlaji na huwezo kula kupindukia kama vile sukari na wanga.

 

Swali la 3: Je Daktari nyama husababisha kansa ya utumbo mpana? Tunashindwa kuelewa vizuri hapa Tusaidie ? 

Nyama imechukua picha kubwa sana kwamba ni kisababishi cha kansa,Mara baada tu ya chapisho ambalo lilitolewa na Shirika la afya duniani tarehe 26 mwezi wa 10, 2015 (Véronique Bouvard, Carcinogenicity of consumption of red and processed meat, 2015) kwamba ni kisababishi cha kansa ya utumbo mpana.

Katika tafiti hii ilikusanya tafiti zaidi ya 800 ambazo zilionesha uhusiano wa nyama na kansa ingawaje baada ya uchunguzi wa kina kuhusu tafiti hizo ,zaidi ya tafiti 744 zilitupiliwa mbali na kuonesha kwamba hazina uhalali wa majibu yake kuchukuliwa kwani njia zilizotumika kiutafiti zilikuwa na mapungufu mengi sana.

Tafiti zilizobaki 56 kidogo ndio ziliweza kukidhi vigezo vya kiutafiti kuweza kujadiliwa zaidi na jopo hilo la wanasayansi. Kati ya tafiti 56, tafiti takribani 27 zilizonesha uhusiano wa nyama ya kusindika na kansa ya utumbo mpana, na tafiti 29 zilikuwa zinaonesha uhusiano kati ya nyama nyekundu ambayo haijasindikwa na kansa ya utumbo mpana. Hapa watafiti walichokuwa wanafanya ni kikubwa sana maana walikuwa wanafanya marejeo ya tafiti zote ambazo zimeshawahi kufanyika duniani zinazo onesha uhusiano wa nyama na kansa.

Katika tafiti 29 zilizokuwa zinazungumzia nyama ya kawaida bila kusindika na kansa baada ya kupitiwa tafiti 15 zilionesha nyama nyekundu sio mbaya na tafiti 14 zilionesha nyama nyekundu ni mbaya, Hapa utaona utata ulivyo mkubwa, Sambamba na hivyo zile tafiti 27 zilizokuwa zinataka kuhakiki kama nyama yakusindika inasababisha kansa ni tafiti 18 zilizo onesha nyama yakusindika mbaya na tafiti 9 zilionesha nyama ya kusindika sio mbaya. Hapa utaona jinsi tafiti nyingi ambazo zilizo onesha ubaya wa nyama ya kusindika. Ndio maana huwa nasema ukitaka kula nyama chagua nyama kutoka kwa ng’ombe anakula nyasi,kutoka sokoni sio nyama ya kusindika.

Baada ya hapa zilibakia tafiti 6 tu ambazo ziliweza kukidhi vigezo baada ya mapitio ya kina, ingawaje chakushangaza tafiti 4 kati ya sita zilifanywa na watafiti walewale yaani aina moja, (Kiutafiti huleta doa kubwa sana,Ingekuwa tafiti hizo 4 na kila tafiti waliofanya ni watu tofauti), lakini tafiti zote 4 ukizipitia zimefanywa na Pierre FH pamoja na Santarelli RL . Ambapo  tafiti 3 zilifanywa kwa kutumia panya, tafiti 2 kwa kutumia binadamu na tafiti moja kwa kutumia panya na binadamu.

Wanasayansi wengi sana walihoji kuhusu hitimisho ambalo Shirika la Afya duniani lilifikia katika tamko lake la mwaka 2015 kuhusu nyama na kansa, hii ni kwa sababu panya wote walio onesha dalili za watu za kansa kilichofanyika ni kwamba, Panya wote waliandaliwa kwa tafiti ya kuangalia kama nyama nyekundu huleta kansa.

Baada ya hapo panya wote wakachomwa sindano inayoharakisha majibu ya kansa, yaani cancer initiator.

Kwa sababu gani huchomwa kemikali hizi kama azoxymethane, Dimethylhydralazine nk ?

Ni kwa sababu itawachukua miaka mingi kusubilia majibu ya mwisho ambayo ni dalili za awali za kansa na tafiti hio itagharimu pesa nyingi sana, kuepusha hilo gharama na muda mrefu panya wote wanachaguliwa ambao wapo hatarini kupata kansa, au wanachomwa kitu kinachosababisha kansa halafu ndipo wanalishwa nyama nyekundu au nyama ya kusindikwa.

Je utajuaje hayo majibu ya muda mfupi uliyo yaona ni kwa sababu ya Nyama nyekundu au ile kemikali uliyowachoma panya? Utata huu ni mkubwa sana katika tafiti zilizo chaguliwa kutoa tamko na WHO.

Ndio maana baadhi ya watafiti na wanasayansi wabobevu katika ugonjwa wa kansa takribani 23 huko Norway  walikaa chini na kupitia tafiti mbalimbali ambazo zinahusisha nyama na kansa mwishoni walihitimisha kwamba,bado kuna mipaka ya utambuzi wa viashiria vya kansa na njia ya utafiti wa uhusiano wa kansa na nyama bado sio nzuri sana hivyo wangeshauri njia zingine zigunduliwe na zitumike. ( Marije Oostindjer; The role of red and processed meat in colorectal cancer development, 2013)

Baada ya tafiti mbalimbali ambazo tumeona zingine nyingi zilikosa vigezo kwa mfano zaidi ya machapisho 800 yaliyokuwa yanataka kutuonesha nyama husababisha kansa ni tafiti 6 tu zilikidhi vigezo vya WHO zingine zote njia zake zilizotumika kufikia majibu kisayansi zilikuwa sio nzuri na zilitupiliwa mbali. Lakini hata hizo sita bado zilikuwa na utata na mambo mengi sana ya kuhoji.  Hayo ndio huendelea katika ulimwengu wa giza, kisayansi kama hujui lakini ukisoma kwa undani yote haya yako wazi kabisa.

Watu wengi sana wakaanza kutafuta mfumo mzuri ambao utawaepusha na kansa ambayo nyama inahusishwa, moja ya tafiti kubwa sana iliyo husisha washiriki takribani 10,998 wasiokula nyama na wanaokula nyama, chakushangaza hakuna utofauti kati ya makundi hayo kwamba kundi la waliokuwa wanakula nyama labda walipata sana kansa. Hapana! (M A Sanjoaquin; Nutrition, lifestyle and colorectal cancer incidence: a prospective investigation of 10 998 vegetarians and non-vegetarians in the United Kingdom, 2004)

Hivyo basi dhana ya kwamba unapokula nyama unakuwa hatarini kupata kansa bado ni kitendawili hadi sasa. Kwa sababu kuna hata baadhi ya tafiti zinaonesha nyama inaweza kukukinga kupata kansa ingawaje unatakiwa kuchagua nyama ambayo haisindikwa kwa kemikali  ( Marije Oostindjer; The role of red and processed meat in colorectal cancer development, 2013)

Kwa nini baadhi ya wanasayansi wanaotaka kuona au kuhakiki uhusiano wa nyama nyekundu na kansa imekuwa kitendawili wameshindwa kuonesha uhusiano?

  1. Wanasayansi wamekuwa wakijiuliza kwamba viini viitwavyo heterocyclic amines na polycyclic aromatic hydrocarbons ambavyo hupatikana endapo ukichoma nyama kwa kutumia moto mkali sana.

Viambata hivi endapo vikichukuliwa vikafanyiwa tafiti kwa panya vimekuwa vikionesha kansa kutokea.

Lakini ukweli ni kwamba hata mboga za majani, hata nyama ya kuku ukichoma kwa kiwango cha moto mkali viini hivi hutengenezeka, na ndio maana wanasayansi wengine wanasema ili viini hivyo viwili viweze kuleta athari kubwa kwenye mwili wa binadamu na kukuletea kansa lazima kiwango chake mwilini mwako kiwe zaidi ya 1,000 hadi mara 100,000 ya kiwango ambacho hupatikana katika chakula chetu cha kila siku.

 

Kibaya zaidi watafiti wanauliza kwa nini nyama ya kuku nayo imeonesha kutengeneza viini hivyo pamoja na samaki lakini hakuna mtafiti ambaye ametaka kuichunguza zaidi nyama nyeupe kuku na samaki? Wanasayansi wengi huwa hawataki kutopata jibu ambalo walitarajia kuanzia mwanzo, ingawaje kiutafiti “Association does not mean causality” unaweza kuhusianisha kitu lakini haimaanishi ni kisababishi, na lengo ya utafiti ni kuhakiki kile ulichofikiria ni ukweli au uongo, sasa wengi hawataki kuonekana kile walichofikiria sio kweli watengeneze nadharia nyingine ili kuendeleza tafiti zaidi.

 

Soma zaidi tafiti hii na inaonesha kwamba “Ili wewe upate kansa kwa kula nyama nyekundu uliyopika au kuchoma yakutaka kwanza uwe na sifa kama za wale panya, uchomwe kitu kinachosababisha kansa, halafu ndipo ule nyama nyekundu na mazingira yanayozuia kansa isitokee yaani uache kula vyakula vya madini ya calcium ndipo utapata kansa” kitu ambacho hakiwezekani kwako. (Fabrice Pierre;Beef meat promotion of dimethylhydrazine-induced colorectal carcinogenesis biomarkers is suppressed by dietary calcium, 2008)

Mbali na hivyo kuna udhaifu mkubwa wa nadharia hii, endapo nyama ukichoma kwa kutumia mafuta yasiyostahimili moto yenye jina la vegetable oil hutengeneza sumu nyingi sana ziitwazo Free radicals na kuuweka hatarini mwili wako kulemewa na free radicals hali hio kitalamu huitwa oxidative stress, tizama tafiti nyingi sana zinaonesha jinsi gani oxidative stress hubadilisha DNA na mitochondria ya seli kuwa kansa kwa uwezo mkubwa sana. Lakini hili hakuna sehemu yoyote linapotiliwa mkazo kwa sababu utakuwa unagusa mafuta yanayofikirika kuwa salama kwa afya zetu kumbe sio kweli.

 

  1. Nyama ambazo zimesindikwa zimekuwa zikionesha kwamba ile dawa ya kusindikia nitrates inapokutana na moto hutengeneza sumu ziitwazo nitrosamine compounds ambazo huhusishwa kusababisha kansa. Hio ndio nadharia yake. Lakini kuna tafiti nyingi zinakanusha na zingine zinakubaliana na dhana hio. Kwa sababu utafiti wa kisayansi sio mashindano ya mpira mwenye pointi nyingi ndiye mshindi lazima zile tafiti chache zitiliwe maanani kufanya tafiti ziendelee kufanyika kujua hasa chanzo chake ni kipi.

 

  1. Hakuna tafiti hata moja ambayo imefanywa kwa vitendo kimaabala, kinachofanyika ni karatasi zinagawanywa kwa walengwa halafu wanahojiwa maswali kadhaa ambayo akiyajibu ndiyo yataashiria kwamba nyama ni chanzo cha tatizo lake. Kwa hio unaposikia tafiti zinasema kwamba “Nyama husababisha kansa” ina maana wale watu waliojibu na kuonekana wanakula nyama mara kwa mara walionekana na dalili za kansa ingawaje mambo mengine kama kitambi,kisukari,vyakula vya sukari na wanga,mafuta mabaya kama prestige,margarine ambayo yanahusishwa kuwa visababishi vya majeraha ya mwili na kansa vinakuwa havijatizamwa na mara nyingi hutuharibia jibu ambalo tumekusudia kumpata adui.

 

Na ndio maana walewale walio onekana nyama wanakula mara kwa mara walikuwa wanakunywa sana pombe, wanakula kupindukia sukari na wanga,wana kitambi,kisukari ni vigumu sana kusema kwamba eti nyama ndiyo ambayo imesababisha magonjwa hayo.

 

Na hakuna tafiti iliyofanyika kwa binadamu wakala nyama pekee bila vihatarishi vingine kama sukari,kiwango cha wanga na mafuta mabaya vikatizamwa kwa umakini,kinacho angaliwa kwa upana ni sigara tu lakini wanga na sukari huwa havitizamwi mbali na kwamba sukari kama kisababishi cha kansa tafiti zinaendelea kuongezeka kila kukicha. Unapokuwa na kitambi,kisukari au mtahiniwa wa kisukari unakuwa hatarini kupata aina mbalimbali za uvimbe,kansa karibia aina zote na ukija kutizama kwa kina maadui hapo ni sukari wanga, margarine nk. Kansa haisababishwi na kitu kimoja, kwa sababu bado hadi sasa hatujajua nini hasa kisababishi cha kansa ndio maana mlipuko wa kitambi kisukari magonjwa haya yanaenda sambamba na mlipuko wa ugonjwa hatari kama kansa. Kinachosababisha kitambi,kisukari yawezekana ndicho husababisha kansa pia. (John Yudkin;sucrose in the diet and coronary heart diseases, 1971)

 

Kumbukumbu zinasema kwamba binadamu ameanza kufuga miaka mingi iliyopita, inakadiliwa mileniumu ya 9 B.C. (Amelie Scheu;The genetic prehistory of domesticated cattle from their origin to the spread across Europe, 2015) . Na inakuwaje leo hii nyama iliyotumika enzi na enzi imegeuka imekuwa hatari kwa afya zetu wakati binadamu ni Yule Yule DNA/Gene yake ni ile ile hajawahi kubadilika? Ukija kuangalia kabla ya mapinduzi ya viwanda tulisaga nafaka kwa mawe, hii ni ishara ya kwamba nafaka,sukari kilikuwa sio chakula kikuu kwetu kama sasa tunavyo ishi hii nadharia inaweza kukupa picha nzuri kutaka kujua kwa nini mlipuko wa kitambi kisukari magonjwa ya moyo yanaenda sambamba na mlipuko wa magonjwa kama kansa.

 

Tafiti zaidi zinahitajika katika nyama, ndio maana mabila mengi sana yamewaacha wanasayansi njia panda kwani chakula chao kikuu ni nyama lakini hawapati magonjwa yote wanayo yahusisha na nyama, ikiwemo wamasai, samburu, Eskimo, Mongolia,shepherd rendille nk. (Shaper AG; Cardiovascular studies in the Samburu tribe of northern Kenya., 1962)

 

 

Wakati Gani Nyama Inakuwa Hatari kwa Afya yako?

Zingatia kwamba Nyama ni moja ya kiambata Muhimu sana katika chakula bora. Na Kiafya ni aina ya chakula chenye Sifa ya Protini kamilifu. Kina Aina nyingi za madini na vitamin, Na Mwili huvuna Viini Lishe kiurahisi kutoka kwenye Nyama (Bioavailability of Nutrients) kuliko kwenye Mimea.

 Sababu zinazoweza kufanya nyama Kuwa mbaya Kwa afya yako:-

  1. Pale ambapo nyama yako Ukichoma au Ukakaanga kwa kutumia mafuta mabaya kama Vegetable oil.

Kwa Mujibu ya Tafiti nyingi Mafuta ya mbegu za mimea yana kiwango Kingi cha Omega 6 kuliko Omega 3 hiki ni kigezo kikubwa sana kwa nini mafuta ya mbegu za mimea yanahusishwa na magonjwa ya kuvimba kwa mwili. [1] [2] na Mbali na hivyo hayastahimili moto sasa unapokaanga au kuchoma kwenye moto mkali unatengeneza Sumu nyingi ziitwazo Kiujumla Free Radicals (Super peroxides  na Aldehydes) [3] . Ambapo Sumu hizi zikiulemea mwili zinakuweka kwenye Msongo wa sumu yaani Oxidative stress ambacho ni chanzo cha magonjwa mengi kama Kisukari,Pumu,Maumivu ya hedhi,Shinikizo la damu,Magonjwa ya moyo,Usahulifu, Pumu ya ngozi (Eczema) nk [4] [5] [6]

  1. Pale Nyama Utakapo Kula ukaambatanisha na Pombe kali. Kwani wengi huhusisha nyama hunenepesha kutokana na mafuta yake lakini hii inatokana na unapokuwa mlaji wa nyama halafu “Ukaambatanisha na Unywaji wa Pombe” [7] [8]
  2. Endapo Ulaji wa nyama ukiambatana na Matumizi mabaya ya Sukari na Vyakula vya wanga.

Hii pia inakuweka hatarini Kupata Kitambi,Kisukari,Shinikizo la damu, nk [9] [10] [11] [12]

Wengi unakuta anatumia nyama Vibaya huku akiambatanisha na Glasi nyingi za Juisi,soda, au Juisi za Kutengeneza Nyumbani. Eating pattern za wengi utakuta “Kaweka nyama,Juisi au soda ,Na Chapati 3” Huo mpangilio sio salama kiafya na Ukisema “Nyama ndiyo imekuuguza Utakuwa una makosa” Lakini endapo “Ukiweka Nyama,Mboga za majani, Matunda umekata kata” na Endapo Ukizingatia Elimu ya Mafuta yenye Sifa kuchomea nyama au Kukaangia nyama Utakuwa Unakula HEALTH kwa mujibu wa #sayansiyamapishi

Pale Unapokula nyama zilizowekewa Kemikali mbalimbali za Kutoharibu ladha ya Nyama. Chagua

nyama ambayo haina Preservative chemicals nyingi  kwa sababu tafiti zinaonesha kwanya nyama nyingi

ambazo zinasindikwa kwa Kuweka nitrates Zinatengeneza sumu nyingi mwilini na zinakuhatarisha

kupata Kansa ya utumbo Mpana.Jitahidi Uchague nyama ya buchani na sio soseji au nyama zingine ambazo sio asili.

 

REJEA ZA SOMO HILI:

[1] Artemis P. Simopoulos, “An Increase in the Omega-6/Omega-3 Fatty Acid Ratio Increases the Risk for Obesity,” Nutrients 8, no. 3 (March 2, 2016), https://doi.org/10.3390/nu8030128.

[2] “Inflammation Omega 3 and Omega 6.Pdf,” n.d.

[3] “Effects of Repeated Heating of Cooking Oils on Antioxidant Content and Endothelial Function – Google Search,” accessed August 30, 2018, https://www.google.com/search?

[4] Karla Cervantes Gracia, Daniel Llanas-Cornejo, and Holger Husi, “CVD and Oxidative Stress,” Journal of Clinical Medicine 6, no. 2 (February 20, 2017): 22, https://doi.org/10.3390/jcm6020022.

[5] “Oxidative Stress-Activated Signaling Pathways,” accessed July 20, 2018, https://www.medscape.com/viewarticle/448389_3.

[6] “Free Radicals Journal.Pdf,” n.d.

[7] Soo-Jeong Kim and Dai-Jin Kim, “Alcoholism and Diabetes Mellitus,” Diabetes & Metabolism Journal 36, no. 2 (April 2012): 108–15, https://doi.org/10.4093/dmj.2012.36.2.108.

[8] “Excessive Alcohol Consumption and Insulin Resistance – Google Search,” accessed July 20, 2018, https://www.google.com/search?q=excessive+alcohol+consumption+and+insulin+resistance&oq=Excessive+alcohol+intake+and+isnulin&aqs=chrome.1.69i57j0.23114j0j4&sourceid=chrome&ie=UTF-8.

[9] Abhimanyu Garg et al., “Effects of Varying Carbohydrate Content of Diet in Patients With Non—Insulin-Dependent Diabetes Mellitus,” JAMA 271, no. 18 (May 11, 1994): 1421–28, https://doi.org/10.1001/jama.1994.03510420053034.

[10] Sharon S. Elliott et al., “Fructose, Weight Gain, and the Insulin Resistance Syndrome,” The American Journal of Clinical Nutrition 76, no. 5 (2002): 911–922.

[11] “Sugar-Sweetened Beverages and Risk of Metabolic Syndrome and Type 2 Diabetes.Pdf,” n.d.

[12] “Gerald M. Reaven, MD: Demonstration of the Central Role of Insulin Resistance in Type 2 Diabetes and Cardiovascular Disease | Diabetes Care,” accessed July 20, 2018, http://care.diabetesjournals.org/content/37/5/1178.

No automatic alt text available.

Afya ni hazina muhimu sana lakini endapo ukikosa elimu ya kina itakuwa rahisi sana wewe kushawishika na mapokeo mengine yasiyokuwa na misingi na ushahidi wa kina. Sayansi ya mapishi imejikita kukupa mwanga na uweze kufanya maamuzi kwa kujua sio kama ilivyo wengi maamuzi juu ya afya ya mwili ni bendera kifuata upepo kwa sababu ya giza nene la ukosefu wa elimu ya kutosha hasa katika maswala ya kitalamu kama haya. Kuwa sehemu ya Gurudumu kunusuru afya yako.

Elimu ya Kisukari imewasaidia Watanzania wengi kwa kutumia Kitabu cha Sayansi ya mapishi sasa nimewaandikia mwongozo maalumu wa vyakula wagonjwa wa kisukari.

Image may contain: 1 person, text

 

Nuru ya Kisukari kitabu hiki nimedhamiria kukupa mwanga wa elimu ya ugonjwa huu, Kinga, na jinsi ya kuukabili ugonjwa huu kwa kuzingatia chakula unachokula. Usipotoke kwa kuambiwa kwamba “Kuugua ugonjwa wa kisukari ni haki yako kwa sababu ndugu zako wengi wana kisukari pia usishangae hakuna ndugu hata mmoja mwenye kisukari ila wewe umeugua kisukari, Pia usipotoke na anayekwambia unaweza kula chochote halafu dawa au mizizi ikatenda miujiza ya kushusha sukari”Ugonjwa wa Kisukari ni ugonjwa wa lishe na tiba yake kwa asilimia kubwa zaidi ya 95 ni Kuzingatia lishe bora anayekwambia upuuze chakula bora tambua kwamba “Unampotezea Muda Daktari wako”

Image may contain: text

Jifunze Elimu ya Kina Ya Kisukari Youtube:

 

Kwa Huduma zaidi: 0767074124 AU 0222760202

ITAPENDEZA SANA BAADA YA KUELIMIKA UKAMTUMIA NA NDUGU YAKO MAKALA HII AKAELIMIKA

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*