HISTORIA: KWA NINI MAFUTA YA WANYAMA YALISEMEKANA MABAYA

Swali: Je Ni kweli Kisayansi Cholestrol (Lehemu) husababisha Magonjwa ya Moyo?

Jibu: Hadi sasa hakuna TAFITI yoyote ambayo Imehakiki kwamba Cholestrol nyingi Husababisha Magonjwa ya moyo. Bali Cholestrol inahusishwa tu na wanasayansi na watafiti.

Kitafiti: Association does not prove causal relationship.

Kihistoria:

 1. Uvumi wa Cholestrol husababisha magonjwa ya moyo. ulitokana na Wanasayansi kutengeneza Dhana ya kwamba “Kwa sababu mafuta ya wanyama huganda hivyo huenda pia ndani ya mishipa ya damu Kuganda. Pia Mafuta haya huongeza Cholestrol na kuziba mishipa ya damu.

 

 1. Hakuna Elimu Yoyote zaidi ya Hapo enzi hizo Watafiti wanahusianisha m/Moyo na Cholestrol sayansi Ilikuwa haijafika mbali. Walitolea mfano kwamba mafuta yanaziba mishipa ya damu kama Uchafu unavyoziba Bomba na maji.

 

 1. Yote hayo hayakuwa na MISINGI na USHAHIDI kisayansi. Kwani kabla ya Elimu hii Binadamu tulikula mafuta ya wanyama na kihistoria mtu wa kwanza kugundulika na magonjwa ya moyo ilikuwa mwaka 1920s.

 

 1. Mafuta ya Mimea (Pamba,Alizeti,Soya,Mahindi) Hayakuwa sehemu ya LISHE yenye kubeba nafasi kubwa kama ilivyo sasa. Kwa sababu teknolojia haikuwepo ya kuvuna mafuta kutoka kwenye Mbegu za mimea. Kwa hio Mafuta haya Hayakutumika enzi na enzi. Lakini Ndio yalikuja kuidhinishwa mwaka 1977 katika Jopo la Watalamu lilioundwa kutengeneza “Dietary Goals for United states” Jopo hili liliongozwa na mwenyeketi Seneta George Mc govern. Seneta Pamoja na Jopo la watalamu wengine Prof Mark Hegested Kutoka chuo kikuu Harvard walikaa kikao cha kuidhinisha hayo Ijumaa,Mwezi wa 1, 1977. Hio ndio Siku Mteule wa Raisi Richard Nixon Katibu wa Idara ya Kilimo amerika George Mcgovern na wana kamati wengine Walitutungia Mwongozo waliosema unaenda Kupunguza magonjwa ya Lishe hasa ya Moyo.

 

 1. Sababu Kubwa Zilizowafanya kuunda Mwongozo wa Lishe mwaka 1977 ni Kupambana na Magonjwa ya moyo, Kisukari, Kitambi nk Pia katika ushauri wao Prof Mark Hegsted alisema “Tena mafuta ya wanyama ni gharama sana ukilinganisha na mafuta ya mbegu za mimea” Pia alisema vyakula vya mafuta Havina kiini lishe chochote ukilinganisha na Chakula cha Wanga. (Profesa wa Nutrition Harvard) Alikuwa anajaribu Kutetea hoja yake kwamba “Mafuta ni mabaya na wanga ni nzuri”

 

 1. Kwa mara ya kwanza Jopo Likapitisha tuanze kula Wanga asilimia 55-60 kwenye Lishe yetu. Kwa mfano: Chukua mfano wewe Unakula Kalori kwa siku 2100. Asilimia 60 ya kalori hizi ni Kalori 1260 na Ukitaka kujua ni sawa na gram ngapi za wanga gawanya kwa 4 (Maana gram 1 ya wanga ikiunguzwa mwilini hutupatia kalori 4) Jibu letu litakuwa gram 315. Kwa lugha nyingine Unashauriwa na mwongozo wa lishe Ule wanga gram ambazo hazipungui 250 hadi 315 kwa siku ili uwe na afya njema. Kiwango hicho wengi husema ni Kikubwa sana (High carb diet) ikapewa dhamana na ikaingia.

 

 1. Vitabu Vilitengenezwa vya mapishi, Mabango yalitengenezwa,Hospital zilitumiwa mwongozo wa lishe na Hapo ndipo Ushauri ukabadilika wote watu wakaanza kuishi katika Kula na kunywa kinyume na Tulivyo ishi hapo nyuma. Kwa sababu gani? Sababu ni “Wale waliohusianisha Mafuta na magonjwa ya moyo” Kuhusianisha mafuta na magonjwa ya moyo haimaanishi NI KISABABISHI. Naweza Kukuhisi unazini na mke au mme wa rafiki yako Lakini haimaanishi ni kweli umezini naye.

 

 1. Katika Mwongozo huo tuliambiwa Kwa mara ya kwanza Cholestrol ni SUMU hutakiwa kula maana inapozidi Mwilini Inakusababisha shambulio la moyo hapo hapo. Tukapewa hadi KIWANGO MAALUMU (Nimetumia herufi kubwa) kwamba Huruhusiwi Kuzidisha gram 300 kwa siku moja. Watu wakapokea ndipo sasa kwa mara ya kwanza “Chakula kikaanzwa kupimwa ubora wake kwa Kuangalia Hicho chakula kina kiwango kiasi gani cha cholestol ndani yake? “Vyakula kama Nazi, Siagi, Maziwa, Nyama vilikuwa kidedea.

 

 1. Nyakati hizo Vyakula vyote vikaanza Kufanyiwa Maboresho halafu NDIPO VIITWE SALAMA kwa matumizi ya Binadamu. Nyama ikaanza kutolewa mafuta kiwandani na Nyama hio ikaitwa “Lean meat” Wao (Amerika) ndio walikuwa na mitambo waliuza Duniani kote. Maziwa yakaanza kuchujwa mafuta na kuitwa “Skimmed milk” Mataifa yetu hayakuwa na teknolojia hio ,Bibi zetu hawakuwa na uwezo huo hata kidogo, Kwa lugha nyingine Vyakula vyote SALAMA TUKAWA TUNAMTEGEMEA AMERIKA . Maana bila yeye Kuboresha nyama,Maziwa Cheese basi TUTAKUWA TUNAKULA CHOLESTROL.

 

 1. Kwa mara ya kwanza Tukakatazwa KULA VYAKULA ASILI. Tukaanza kula vyakula vilivyo Boreshwa na Amerika na Kuitwa vyakula vizuri na salama kwa afya yako.

 

 1. Sambamba na Kuwekewa Ukomo wa Kiwango cha CHOLESTROL kwamba Usizidishe gram 300 kwa siku. Tukaambiwa mafuta ya Wanyama kama Siagi (Butter), Samli (Ghee), Tallor (Mafuta ya ng’ombe” na Nazi Yana kiwango kingi sana cha Cholestrol hutakiwi kutumia yanakuweka hatarini kupata magonjwa ya moyo. Matangazo mbalimbali na Mapishi mbalimbali yalipikwa kwa Mafuta ya mbegu za mimea yalisambazwa duniani kote vitabu viligawiwa bure na matangazo kwenye TV yalikuwa ya kishindo( Marketing strategies) zilikuwa na nguvu ya aina yake.

 

 1. Kwenye TV moja ya Tangazo ambalo liliwatisha Amerika video ya katuni iliyosema “ A great boom to american’s arteries, Don’t Eat butter”. Yaani TV zote zilionesha Ubaya wa Mafuta ya Wanyama jinsi yalivyo hatari katika mishipa ya damu. Na Mwishoni Video ilionesha inasema “Mbadala wake kula mafuta yatokanayo na mimea” Kipindi hicho yakikuwa mafuta ya Pamba maarufu kama CRISCO kirufu chake ni Crystallized Cotton Oil ,Mafuta haya yalichukuliwa mafuta ya Pamba yaliboreshwa zaidi kwa mujibu wao na kitendo hicho huhusisha kuyachoma mafuta ya pamba(PUFA) katika moto mkali kwa kutumia hata kemikali kama Nickel catalyst kuyabadilisha yawe kama mafuta ya wanyama (Mgando). Kitendo hicho huitwa Hydrogenation. Ndivyo Mafuta yote ya mgando yatokanayo na mimea yanavyo tengenezwa. Soma Mafuta yote yanayo itwa margarine sokoni utagundua.

 

 1. Tumetumia mafuta hayo ya Margarine (Hydrogenated Vegetable oil) yaliyo tolewa sifa kuu na kamati hio kwamba “Yana bei Rahisi,na miili yetu mfumo wa chakula humeng’enyw vizuri” Kwa miaka 30 baadae Mafuta haya ya mimea yalichukua soko la mafuta ya wanyama.

 

 1. Kihistoria Amerika ilianza Kulima Pamba mwaka 1736. Na Wakati huo Pamba ilitumika kwa asilimia kubwa kuchukua Sufi (Fiber) na kutengenezea Nguo. Wakati mbegu zilitupwa,Zilikuwa mbolea na hatimaye chakula cha wanyama.

 

 1. Kilimo cha Pamba kilikuja kushamiri Amerika mwaka 1793 baada ya Ugunduzi wa Mashine ya Kuchambua Pamba (Yakutenganisha mbegu na Sufi ). Uzalishaji ulitoka kilo 300 mwaka 1784, 100,000 mwaka 1780 na mpaka kilo 20,000,000.
 2. Katika Pamba hio mbegu zilikuwa nyingi sana na asilimia chache sana zilitunzwa kwa ajili ya “Mbegu” nyingine zilibaki hazina kazi Yoyote.

 

 1. Kampuni maarufu duniani enzi hizo ya Procter na Gamble wakabuni namna ya kutumia Mafuta ya Pamba kutengeneza Sabuni na mishumaa. Kwa sababu Walikuwa wanatumia gharama kubwa sana kutengeneza sabuni na mishumaa kwa kutumia mafuta ya wanyama kwa sababu ya bei zake kubwa.

 

 1. Kampuni hio ya Procter na Gamble ilifanikiwa kutengeneza mafuta kwa mara ya kwanza ya Pamba yalikuwa mekundu sana na radha chungu. Hii ilitokana na kiambata moja wapo ndani ya mafuta ya pamba kilijulikana kama “Gosspol” kilikuwa ni sumu kali chenye kuangamiza figo,Kupandisha madini ya Potasium (K+) na Kuumiza viungo mbalimbali ndani ya mwili. Ilibidi wagundue njia ya Kuondoa sumu hio ndani yake kwanza.

 

 1. Kampuni ya William Procter na James Gamble ilianza kufanya haya mwaka 1870s baada ya Mtikisiko mkubwa wa kiuchumi Amerika. Gharama za Mafuta ya kula (Wanyama yalipanda sana) na Gharama za Sabuni Zilipanda sana. Maana sabuni walitengenezea Mafuta ya Wanyama sio Mimea.

 

 1. Procter na Gamble waliweza kufanikiwa kutengeneza Mafuta ya Pamba na Kuyafanya yafanane na mafuta ya wanyama kwa lengo yawe mbadala kwenye kutengeneza Sabuni na Yaweze kuwa mbadala hata kwa Kupikia.

 

 1. Mwaka 1910 Procter na Gamble waliweza kufanikiwa kutengeneza Bidhaa yao ya Mafuta yanayo FANANA na Mafuta ya Wanyama kwa kusaidiwa na mkemia Edwin Kayser Mjerumani Mwaka 1907(Aligundua njia ya kubadilisha mafuta ya Pamba yawe na Mfanano kama Mafuta ya wanyama) yakapewa jina la CRISCO. Yaani Crystallized Cotton oil. Baada ya hapo kampuni hii ilianza Kufikiria Namna ya Kuyaingiza Sokoni Yakashindane na Mafuta ya enzi na enzi yaani Kama Siagi, Nazi Samli nk Waliamua Kujikakamua kibiashara wakatumia Kampuni Iliyokuwa Vizuri sana sana Katika Masoko kampuni hio ni J Walter Thompson Agency. Hii inamiliki wasanii wote wa nyimbo, Inamiliki waandishi wote na ilikuwa rahisi kufikisha ujumbe haraka sana. Waliwatumia wasanii, waandishi na walituma Barua pepe au Emails Hospital kubwa zote, Kwa madaktari maarufu wote,Kwa watalamu wa lishe wote maarufu na waligawa vitabu vya Mapishi bure vyenye kuonesha unaweza Kupikia “Crisco (Pamba) na sio mafuta ya wanyama”

 

“What was garbage in 1860 was fertilizer in 1870, cattle feed in 1880, and table food and many things else in 1890.”

 

“Kilichokuwa Uchafu mwaka 1860, Mbolea mwaka 1870 na chakula cha wanyama mwaka 1880 Kikawa chakula salama kwa afya kuanzia mwaka 1890 na Mwaka 1910 kikaingia sokoni kwa kishindo na Matangazo mazito”

 

 1. Mafuta mengine yakaanza Kufuata Kama Soya, Kumbuka kilimo cha Soya kilikuwa maarufu sana China miaka ya 7000BC lakini China Ilikuwa haina teknolojia hio ya kuvuna mafuta. Asilimia 18 ya mbegu ya soya ndio huwa mafuta. Hivyo Ilikuwa kazi sana Kuyapata mafuta yake. Lakini Amerika ya kazikazini ilianza Kutilia mkazo kilimo cha soya mwaka 1765 na ndipo Uzalishaji ulivyokuwa mkubwa Mafuta ya Soya yakagundulika na tukaanza kushauriwa ndio mafuta salama mbadala wa mafuta ya wanyama.

 

 1. Kwa mara ya Kwanza Duniani TAASISI YA MOYO AMERIKA iliundwa mwaka 1924 ingawaje haikuwa IMARA KAMA SASA NA YENYE KATIBA ZA UENDESHAJI. Enzi hizo walikuwa wanakutana tu Jopo la Madaktari wachache wa Moyo na Kujadili. Kwa sababu Haikuwa na Pesa kabisa za Kujiendesha.

 

 1. Mwaka 1948 Kampuni ya William Procter na James Gamble iliyokuwa inayasukuma kwa Nguvu zote mafuta ya CRISCO Yatokanayo na Mbegu za Pamba Walifadhili Taasisi hii kwa dola 1.5 milioni (Donation , au donge la pesa kutoka kwa Procter na Gamble company)

 

 1. Mwaka 1957 Ancel Benjamin Keys Daktari bingwa na mtalamu wa Viumbe Samaki alichomoza na kutaka kufanya tafiti kwa binadamu “Akihusisha Mafuta ya wanyama,Cholestrol na Magonjwa ya moyo” alishirikiana na watafiti kutoka Chuo kikuu cha Harvard. Wakafanya Tafiti kwa kuzunguka Nchi 22 wakaja wakatoa majibu Nchi Saba tu zingine zote 15 alizitupilia mbali takwimu zake. Akafoji majibu ya tafiti yake kwa Kutoa takwimu za nchi Saba badala ya 22. Wana sayansi Walipinga na wakachukua takwimu hizo hizo zake alizokusanya nchi zote 22 walipochora graph Hakuna uhusiano wa mafuta na magonjwa ya moyo ulionekana. Alifanya hivyo Ili KUPATA JIBU AMBALO ALIKUSUDIA KABLA HATA YA KUFANYA TAFITI. Soma zaidi Tafiti inaitwa SEVEN COUNTRIES STUDY (SCS).

 

 1. Mbali na watafi na Wanayasansi Kukataa Tafiti hio, Lakini mwaka 1961 Taasisi ya Moyo Amerika Ikaidhinisha Rasmi kwamba “Mafuta ya Wanyama mabaya, Tule mafuta ya Mbegu za mimea kipindi hicho yalikuwa ni Crisco”. Hili tukio lilifuata baada ya mwaka 1924 Gamble na Procter kuwa wadhamini Wakuu wa Shirika hili.

 

 1. Mwaka 1970s Raisi wa Amerika akatengeneza Jopo au kamati ya Kutengeneza Mwongozo Wa Lishe ili Amerika Ifuate na moja ya mambo ya muhimu yalikuwa ni “Kuongeza matumizi ya wanga hadi asilimia 55-60 ya nishati unazishiba zitokane na wanga (Wanga ikahalalishwa ni chakula bora). Na Mafuta yanayoganda yawe chini ya asilimia 10 na hutakiwi kuzidisha mafuta zaidi ya asilimia 30. Cholestrol kwa siku Marufuku kuzidisha gram 300. Hayo Yote yalipitishwa na mwenyeketi wa jopo hilo “Dietary Goals for United states” Tarehe 14,Mwezi 1 Mwaka 1977 siku ya Ijumaa.

 

 1. Kwa lugha nyepesi Vyakula Vyote vya wanyama vikawa ni “Hatari kwa afya” na vyakula vyote vya “Nafaka,ngano na mafuta ya mimea” vikawa salama kiafya.

 

 1. Hadi sasa Kuna Tafiti zakutosha zinazokanusha kwamba Cholestrol sio kisababishi cha magonjwa ya moyo. Hata hivyo zaidi ya nusu ya wanaopata shambulio la moyo kiwango chao cha cholestrol hakipo juu. Pia tafiti zinasema kwamba Cholestrol pekee kuwa juu haiwezi kujitosheleza kusababisha upate shambulio la moyo. Kuna stori ndefu na vihatarishi vingine.

 

 1. Pia kuna tafiti za kutosha zinazo onesha kwamba magonjwa ya moyo sio magonjwa ya cholestrol, Ni Magonjwa ya Mashambulizi ya kuta za mishipa ya damu. (Inflammatory diseases and not Cholestrol diseases). Hii ni kwa sababu Bila majeraha katika mishipa ya damu cholestrol haiwezi kuleta athari zozote katika mishipa ya damu.
 2. Tafiti Pia zinaonesha kwamba vihatarishi vya majeraha katika mishipa ya damu ni pamoja na Sumu za Sigara, Sukari, Wanga, Stress (Msongo), Mafuta ya Omega 6 kwa wingi. nk Kwa maana hio maadui wakubwa ambao tunatakiwa tupambane nao sasa ni “Sigara, Pombe, Sukari, Wanga Kupindukia,Msongo wa mawazo, Mafuta ya mbegu za mimea (Pamba,alizeti,Soya,Mahindi) nk

 

 1. Kwa sababu Hizo na tafiti nyingi kwa mara ya kwanza ikiwa ni miaka zaidi ya 35 tangu mwongozo wa Lishe Utengenezwe ambao ndo tunatumia duniani kote kurejea. Mwaka 2015 wakati wa kamati inakaa kurejea tafiti zinasema nini kuhusu Mwongozo wa lishe walikubaliana kwamba “KUONDOA UKOMO WA CHOLESTROL”. Yaani Miaka yote hio Tunaambiwa “Cholestrol kwenye chakula ni sumu, Ondoa kabisa na kula vyakula ambavyo havina cholestrol” Ila Mwongozo wa mwaka 2015 -2020 unasema kwamba “Tumeamua kuondoa UKOMO wa Cholestrol Unayotakiwa kula kwa siku ila Haimaanishi Ule Kwa uhuru endelea kuwa na Woga hivyo hivyo”. Inabidi ucheke tu. Yaani Kitu ambacho ni Hatari kwa afya yako Umewekewa ukomo miaka na miaka mpaka dawa za kushusha cholestrol viwanda vikawa vinaondoa mafuta kwenye vyakula asili, Viwanda vikaamrishwa kuandika Cholestrol free leo hii Jopo linakuja na Mwongozo mpya “UKOMO WA CHOLESTROL SASA UMEONDOKA”

 

 1. Kwa sisi wachambuzi na wafuatiliaji wa mambo haya ni Neema kubwa sana. Ipo siku Ukweli utawekwa wazi kuondoa tu ukomo juu ya cholestrol ni hatua kubwa imepigwa na yote ni kutokana na TAFITI NYINGI wanazotumia Pesa nyingi Kuhakiki Uongo zinagonga mwamba, Upande mwingine Tafiti nyingi zinaonesha kwamba “Cholestrol pekee sio kisababishi cha magonjwa ya moyo Moja kwa moja”. Kama Ukomo Umeondoka Je Dawa za kushusha cholestrol nazo tutarajie zitaondoka? Sitaki Kwenda huku tunasubiria Mwongozo Ujao.

 

 1. Hakuna sehemu Yoyote kwenye Vitabu vya Biochemisty au kemia ya vyakula vinavyo onesha kwamba Saturated Fat inabadilika kuwa Cholestrol Hakuna hio Kitu. Ila aliyetuambia hayo “Alihusianisha” Kwamba Ukila vyakula kama Nyama,Mayai, Siagi samaki unaongeza Cholestrol. Vitabu vingi vinaonesha dhahiri kwamba asilimia zaidi ya 80 ya cholestrol hutengenezwa na mwili wako binadamu. Na ni asilimia 20 tu ya mwili hutegemea cholestrol kutoka kwenye chakula unachokula. Chanzo Kizuri cha cholestrol ni mwili wako na sio Chakula. Kama Cholestrol ni mbaya unaambiwa kwamba Hata kama usipokula chakula cha cholestrol mwili utatengeneza Kufidishia lile gepu ambalo linapelea ili kukidhi mahitaji ya mwili. Na unaambiwa ukila chakula cha cholestrol mwili huwa unatambua hilo na hatimaye hupunguza uzalishaji wa cholestrol ndani ya mwili. Chakula hubadilisha cholestrol kwa kiwango kidogo sana kwenye damu.

 

 1. Usipumbazike kwamba cholestrol katika chakula ni sawa na cholestrol inayo ingia kwenye damu. Huu ni Upotoshaji mkubwa sana kibaolojia na sayansi ya umeng’enyaji wa chakula cha mafuta na cholestrol inapingana na imani hio ya wengi.

 

 1. Wengi hawajui kwamba bila cholestrol Uhai wako unatoweka mara moja. Yaani endapo nikifanikiwa kuifanya cholestrol ikawa chini ya kiwango karibia ziro Unapoteza maisha hapo hapo. Cholestrol ni uhai. Unakumbuka Sayansi ya Kidato cha kwanza? Cell is a basic unit of Life? Kila sekunde mamilion ya seli yanakufa na zinatakiwa kutengenezwa mpya, Na kumbuka unapokua Utengenezwaji wa seli unatakiwa uwe mkubwa kuliko kufa kwa seli, Hio hali ndo Inakupa Ukuaji. Na seli ili itengenezwe mali ghafi ni Cholestrol.

 

 1. Haya unakumbuka tulifundishwa baolojia ya kidato cha tatu kuhusu “Mfumo wa neva za Fahamu” kwamba ili umeme usafiri kwa kasi ya ajabu unahitaji “Axons, Nyaya za mfumo wa fahamu zifunikwe na mafuta yaani myelin shealth” sawa na nyaya za Umeme wa Tanesco zimekuwa insulated kutokupoteza Umeme. Ndivyo hivyo hivyo hata mfumo wa umeme wa mwili Nevu za fahamu zimegunikwa na cholestrol huitwa myelin shealth ambayo huongeza ufanisi wa mfumo wa nevu za fahamu. Ndio maana Tafiti zinaonesha kwamba vyakula kama mayai, Samaki, Nazi vinaweza Kukupunguzia kasi ya kuzeeka haraka yaani ni ant aging” Wakati Ngano, Nafaka, na Mafuta ya mbegu za mimea (Omega 6 rich oils) yanahamasisha Uzee na magonjwa ya uzee (degerative diseases)

 

 1. Mbali na Hivyo Mafuta hutembea na vitamin A, D E na K . Kwa pamoja huitwa Fat soluble vitamin. Vitamin hizo mfano A inapatikana kwa wingi kwenye vyakula vya wanyama tofauti kabisa na wengi wanavyojua kwamba matembele,karoti ndio ina vitamin A nyingi kuliko Mayai, Maziwa ,samaki na nyama. Ndio maana tunaziita ni “Fat Loving Vitamin”. Leo hii Jamii inateseka na Upungufu wa vitamin A,D,E na K kwa sababu ya Mwongozo wa Lishe unaotuambiwa chakula salama ni Nafaka,Ngano na mafuta ya mbegu za mimea ambayo sio chanzo Kizuri cha vitamin hizo. Ukitaka Usipatwe na magonjwa ya Upungufubwa vitamin Hizo labda Uwe na vidonge mkononi vya Vitamin hizo au Ule vyakula ambavyo vina vitamin hizo Naturally. Soma mafuta mengi ya mbegu za mimea yamekuwa “Fortified na Vitamin A na Vitamin Zingine kama E” Kwa nini? Kwa sababu Wanajua Tunapungukiwa kwa sababu ya Low Fat Propaganda.

 

 1. Tutaendelea Kujifunza Tafiti moja baada ya nyingine. Faida za Cholestrol katika mwili wa binadamu ni nyingi sana hata ili binadamu tuendelee kuzaliana cholestrol inahitajika. Maana bila cholestrol huwezi kukidhi mahitajiya kutengeneza Homoni za kiume na kike yaani Testostorone na Estrogen, Progesterone nk Kwa maana nyingine “Cholestrol inatuhakikisha mwendelezo wa kizazi na kizazi” Labda yawezekana ndio maana Mwili wako Unetengenezewa uwezo mkubwa wa kutengeneza Cholestrol zaidi ya asilimia 80 hata kama Usipokula vyakula vya Cholestrol. Na hatuwezi Kutumia dawa za Kushushw cholestrol kama kujikinga na magonjwa ya moyo tafiti zinaonesha kwamba zinatuhatarisha na mengine na athari zake ni kubwa zinapotumika kwa mtu ambaye hajawahi kupata shambulio (Primary prevention) kidogo zina msaada kwa wenye stroke, Shambulio la moyo tayari ili kuwazuia wasipatwe tena (Secondary Prevention)

 

 1. Amerika Ilifuzu Kuingia kwenye mapinduzi ya viwanda Ikiwa ni bara la kwanza Kulika pamba nyingi na kutengeneza mafuta ya pamba, Kulika soya na kutengeneza Mafuta ya soya ,Kulika mahindi mengi na kutengenezw mafuta ya mahindi halafu kuyahalalishw mafuta hayo ni salama kwa afya ya binadamu kwa kutumia mgongo wa wanasayansi. Na akafanikiwa Kuyapoteza mafuta ambayo yalitumika enzi na enzi Mafuta ya Ng’ombe, Samli,Siwgi na Nazi.

 

 1. Sasa Inapata Taabu sana kutaka Kutuaminisha Hawakufanya makosa hayo ya Kimakusudi. Ila tunashukuru Mwongozo umesema “Hakuna ukomo wa cholestrol tena” Kile kiwango cha gram 300 kwa siku cha cholestrol hakipo tena. Hii ina maana kwamba “Ipo siku katika Jopo hilo watashindwana au watatokea vijana wenye ukweli kwamba mafuta ya mimea sio salama kiafya kama tulivyo aminishwa kwa miaka 35 na zaidi. Cholestrol sio adui tena na maadui watawekwa wazi wanaotufanya tuwe watumwa wa madawa ya magonjwa ya lishe kila siku.

 

Je mafuta ya Nazi ni sumu? Kwa mujibu wa Prof Karin Michels wa chuo kikuu Harvard?

 

Professor Harvard: Mafuta ya Nazi ni Sumu, Katika video yake Imezua Gumzo kubwa sana Duniani ila Yawezekana ni Mtizamo wake Binafsi sio La Jopo la Wanasayansi Wote duniani.

 

“Kwa mujibu wa Mwongozo wa Lishe mwaka 2015-2020 Ukomo au Kizuizi cha kiwango cha Cholestrol kwa siku 300mg Umeondolewa”

 

Kwa miaka zaidi ya 35 tuliaminishwa “Cholestrol ni hatari kiafya usizidishe gram 300 kwa siku. Ila sasa Ukomo Umeondolewa katika mwongozo Mpya wa amerika. Umesema “Tumeamua kuondoa ukomo wa cholestrol”

 

Hebu Jiulize Kitu ambacho ni Hatari kwa afya tumeimbiwa kwaya wee, Tumetengeneza dawa za kushusha cholestrol weee,Tumebadilisha vyakula vikaitwa low fat,Skimmed milk,Cholestrol free,Lean meat, egg white,Skinneless chicken mwisho wa siku wanaondoa UKOMO. Nini Maana yake?

 

UKWELI UMEANZA KUJIDHIHIRISHA KWAMBA “CHOLESTROL SIO KISABABISHI CHA MAGONJWA YA MOYO” Ipo Siku Dunia nzima Itatikisika na Viwanda Vitatikiswa siku wakisema waziwazi.

 

Najua hata wewe HUJAUSOMA MWONGOZO WA LISHE KASOME UONE INGIA GOOGLE UTAFUTE NA USOME WOTE. Mtanzania Anakabidhi Maisha yake kwa Kutokuwa na Tabia ya kujisomea hata vitu vidogo vidogo kama Hivi. Be concerned na afya yako Hakika hutaugua hovyo hovyo Magonjwa yanayo Epukika.

 

Sasa Mbali na Mwongozo wa Lishe kuanza Kukiri wazi na kuondoa Ukomo wa Cholestrol kuna Baadhi ya wanayasansi na Taasisi huwa “HAZIKUBALI KUKIRI KWAMBA JAMANI EEE TULIFANYA KOSA KUHUSIANISHA CHOLESTROL NA MAGONJWA YA MOYO”

 

Ndio Huyu Profesa anaendelea na Kusimamia Kile ambacho KIMESHA KUWA PROVEN WRONG.

 

Katika Video hio inayo sambaa huyo Daktari kasema kwamba “Mafuta ya nazi yanaongeza LDL-C kitalamu ni kibebeo cha cholestrol ambacho hupeleka cholestrol kwenda kwenye mishipa ya damu. Na kwa hio kazi yake LDL-C nyingi huhusishwa na Uhatari wa magonjwa ya moyo.

Ingawaje Tafiti ya kimaabara iliyofanyika kwa kuwatenga watu katika makundi matatu na kuwapa mafuta ya nazi mzeituni na Siagi (Butter) gram 50 kwa muda wa wiki kadhaa chakushangaza ni kwamba Uwezo wa Mafuta ya nazi gram 50 na mafuta ya Olive oil gram 50 katika kupandisha LDL-C inayo husishwa na uhatari wa magonjwa ya moyo Effect yake ilionekana ni sawa hakuna utofauti.

 

Tafiti hio hii hapa unaweza kuisoma yote kwa kina [1] ( ‘Randomised Trial of Coconut Oil, Olive Oil or Butter on Blood Lipids and Other Cardiovascular Risk Factors in Healthy Men and Women | BMJ Open’ <https://bmjopen.bmj.com/node/133027.full> [accessed 27 August 2018]. )

 

 

Mbali na hivyo Tafiti iliyofanywa na Prof Uffe Ravnskov mtafiti na Mbobevu wa Cholestrol alitizama Vipimo vya tafiti zilizojumuisha watu milion 2 kuangalia kama kuna uhusiano kati ya LDL-C na Magonjwa ya Moyo kwa watu wazima. Kilicho mshangaza “Hakuna Uhusiano na Tafiti ilionesha kinyume chake” Kwamba waliokuwa na LDL-C Nyingi Walionekana kuishi Umri mrefu.

 

Soma Tafiti hio kwa kuisoma yote hapa[2] ( Lack of an Association or an Inverse Association between Low-Density-Lipoprotein Cholesterol and Mortality in the Elderly: A Systematic Review | BMJ Open’ <https://bmjopen.bmj.com/content/6/6/e010401> [accessed 27 August 2018]. )

 

Mbali na Hivyo Nazi Inaongeza HDL-C ambayo wengi tunaita kwa jina maarufu kama cholestrol nzuri.

Harvard bado Wanatumia Nguvu nyingi sana Kupotosha Jamii vitu vingine Vimegonga mwamba “Tafiti anayo husianisha kwamba nazi Huongeza LDL-C ambayo ndio wengi huita cholestrol mbaya zimekanushwa na Tafiti nyingi.

 

Tafiti niliyo ambatanisha inaonesha “Olive oil ina uwezo sawa na Nazi kwenye kupandisha LDL” Kwa hio Uhusiano huo Hauna maana yoyote. Kwa maana hio hata Olive oil nayo kwa sababu Tafiti za maabara zinasema ina uwezo sawa nayo ni mabaya?

 

Kama hoja ni kwamba Mafuta yanayo ganda ndani ya nazi ndio ubaya wa nazi, Hilo lishapingwa vikali kutokana na Mapungufu ya Mwongozo wa Lishe wa mwaka 1977.

Soma Mtafiti aliyejikita kutafiti mwongozo wa lishe jinsi alivyokosa Ushawahidi wa kutosha kwa nini Mafuta yanayo ganda ni hatari kwa binadamu wakati maisha ya enzi kabla ya mafuta ya mimea yalitumika na tulikuwa ndiyo sehemu ya Lishe ya babu na bibi zetu.

Soma Hapa zaidi:

 

 1. Tafiti za kimaabara zilizotumika kuunda mwongozo wa Lishe nazo hazikuonesha ushahidi kwamba “mafuta yanayo ganda ni hatari”

 

Soma Tafiti za Marejeo hapa[3] ( ‘Evidence from Randomised Controlled Trials Did Not Support the Introduction of Dietary Fat Guidelines in 1977 and 1983: A Systematic Review and Meta-Analysis | Open Heart’ <https://openheart.bmj.com/node/135594.full> [accessed 27 August 2018]. )

 

 1. Tafiti za Kutumia Watu nazo ziligoma kuonesha ushahihidi huo

Soma Tafiti yote hii hapa[4] ( ‘Evidence from Prospective Cohort Studies Did Not Support the Introduction of Dietary Fat Guidelines in 1977 and 1983: A Systematic Review | British Journal of Sports Medicine’ <https://bjsm.bmj.com/content/51/24/1737> [accessed 27 August 2018]. )

 

 1. Tafiti zingine zilizo rejewa na kuonesha hakuna ushahidi ni hii hapa soma yote[5] (‘Evidence from Randomised Controlled Trials Did Not Support the Introduction of Dietary Fat Guidelines in 1977 and 1983: A Systematic Review and Meta-Analysis | Open Heart’ <https://openheart.bmj.com/node/135594.full> [accessed 27 August 2018].

 

 

 

 

 

 1. Mwandishi mashuhuri na mtafiti Nina Techoiz alifanya marejeo ya tafiti zote za Mwongozo wa lishe “Mafuta yanayoganda ni mabaya, Mafuta ya alizeti pamba soya mahindi ni mazuri, Wanga asilimia 55-60” Kilicho mshangaza Hakuna ushahidi wakutosha kuhusu Mapendekezo hayo yote.

Soma tafiti Yote hii hapa[6] (‘The Scientific Report Guiding the US Dietary Guidelines: Is It Scientific? | The BMJ’ <https://www.bmj.com/content/351/bmj.h4962> [accessed 27 August 2018].)

 

Kwa Hio Kama mafuta ya nazi “Ubaya wake ni kwamba mafuta yanaganda hilo kitafiti limekanushwa vyakutosha na Hakuna ukweli wowote kwamba mafuta yanayoganda husababisha magonjwa ya moyo”

 

Soma hizo Tafiti na Utambue kwamba tafiti za afya au zozote sio Mashindano ya mpira kwamba mwenye Point nyingi ndiye anayeshinda. Hapana hata kama kuna Tafiti moja Inakinzana na hypothesis yako Unatakiwa kurudia tena. Ndio maana Tafiti kubwa duniani zimejaribu kuhakiki na kutuaminisha “Saturated fat is bad zimeishia kupoteza pesa na zimeshindwa”

REJEA ZA SOMO HILI

 

[1] ‘Randomised Trial of Coconut Oil, Olive Oil or Butter on Blood Lipids and Other Cardiovascular Risk Factors in Healthy Men and Women | BMJ Open’ <https://bmjopen.bmj.com/node/133027.full> [accessed 27 August 2018].

[2] ‘Lack of an Association or an Inverse Association between Low-Density-Lipoprotein Cholesterol and Mortality in the Elderly: A Systematic Review | BMJ Open’ <https://bmjopen.bmj.com/content/6/6/e010401> [accessed 27 August 2018].

[3] ‘Evidence from Randomised Controlled Trials Did Not Support the Introduction of Dietary Fat Guidelines in 1977 and 1983: A Systematic Review and Meta-Analysis | Open Heart’ <https://openheart.bmj.com/node/135594.full> [accessed 27 August 2018].

[4] ‘Evidence from Prospective Cohort Studies Did Not Support the Introduction of Dietary Fat Guidelines in 1977 and 1983: A Systematic Review | British Journal of Sports Medicine’ <https://bjsm.bmj.com/content/51/24/1737> [accessed 27 August 2018].

[5] Zoë Harcombe, Julien S. Baker, and Bruce Davies, ‘Evidence from Prospective Cohort Studies Does Not Support Current Dietary Fat Guidelines: A Systematic Review and Meta-Analysis’, Br J Sports Med, 51.24 (2017), 1743–49 <https://doi.org/10.1136/bjsports-2016-096550>.

[6] ‘The Scientific Report Guiding the US Dietary Guidelines: Is It Scientific? | The BMJ’ <https://www.bmj.com/content/351/bmj.h4962> [accessed 27 August 2018].

1 Comment

Leave a Reply to Anno Pius Cancel reply

Your email address will not be published.


*